Thursday, March 19, 2009

MSIBA SALEM

WATANZANIA NA WAKENYA WA CHENNAI WAFANYA IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU EVELYN KARUMBA ALIYEFARIKI HUKO SALEM, TAMIL NADU.....


Evelyn alikuwa mwanafunzi mkenya aliyesomea physiotherapy huko Salem. Alikuwa amemaliza internship yake baada ya kumaliza digrii yake na alitazamiwa kurejea kwao Kenya siku ya jumapili tarehe 15, siku tuliyoadhimisha ibada ya kumuaga.

Kulingana na taarifa tulizozipata kutoka kwa rafiki yake Yasinta, Marehemu aliugua kwa kipindi kifupi kabla ya kufariki akielekea hospitali huko Salem. Taarifa zilizotokana na Post-moterm zinaonesha marehemu alifariki kwa sickle-cell anaemia.

Evelyn alizikwa kwao Kenya ijumaa ya tarehe 13 Machi.

Atakumbukwa kama rafiki mpole na mkarimu mwenye msimamo na mkweli kwa rafiki zake. Mungu amlaze mahala pema.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya mawasiliano,
Jumuiya ya watanzania,
Tamil Nadu.

No comments:

Post a Comment