Majira ya saa 3 na nusu wanajeshi wanaosemekana kutoka kambi ya anga ya Ngerengere na kikosi ya Nyumbu, Msangani walivamia eneo la ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Rais Jakaya Kikwete alitegemewa kuwa na Hafla kwa heshima ya Muwakilishi wa Malkia wa Uingereza Gavana Quentin Bryce wa Australia
Wanajeshi hao wanasemekana kupanga njama za kuzima umeme wa eneo zima la ocean road na feri ambapo ofisi muhimu za serikali zipo. Mpaka hivi sasa haijafahamika kama wafanyakazi wa shirika la umeme nchini TANESCO walihusika kwenye njama hizo.
Mpaka tunaingia mitamboni haijafahamika Rais Kikwete yuko wapi kwani wanajeshi hao waasi hawajathibitisha kumtia nguvuni. Hata hivo inasadikika Rais alipata nafasi ya kutoroka kama ilivyokuwa katika mapinduzi ya mwaka 1964 ambapo baba wa taifa alifanikiwa kuwaponyoka waasi walipovamia ikulu.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa wametoa maoni yao kuhusu tukio hili huku wengi wao wakisisitiza kuwa sio jambo la ajabu sana kwani wimbi la mapinduzi limeonekana kuliteka bara la Afrika katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Kulingana na maelezo yao inawezekana wanajeshi wa Tanzania wameamua kuiga mfano wa wenzao waliotangulia na inawezekana mapinduzi haya yakaendelea katika nchi zingine. Imethibitika kuwa hali ngumu za kiuchumi, kupanda mno kwa gharama za maisha na kushuka kwa maadili katika jamii ndio vimekuwa vichocheo vikubwa katika bara la Afrika kwa kipindi hiki.
Wakati ukisoma habari hii kumbuka leo ni siku ya wajinga duniani na WAJINGA NDIO WALIWAO.

No comments:
Post a Comment