Saturday, April 11, 2009

SALAAM ZA PASAKA

Ndugu watanzania wenzangu, Nachukua nafasi hii kuwatakieni nyote kheri na fanaka tele za sikukuu hii ya pasaka. Naamini Pasaka kama zinavoweza kuwa sikukuu nyingine zozote za kidini inatupa nafasi muhimu ya kutuunganisha sisi watanzania na kujumuika.

Naomba kuwaalika nyote kutumia nafasi hii muhimu kukuza ushirikiano baina yetu watanzania bila kujali dini zetu. Kama ambavyo tungeweza kuunganika wote kwenye tafrija ya kusherekea Eid el Hajj  basi vivo hivo tutumie nafasi hii kama watanzani kwenye miji yetu kukusanyika na kujumuika. Nawasihi kuendelea kuukuza moyo wa ushirikiano tulionuia kuujenga kupitia jumuiya yetu.

Naamini wote kwa namna moja au nyingine tutapata furssa ya kusherekea sikukuu hii. Tukumbuke basi kuwashirikisha watanzania wenzetu katika kuadhimisha sikukuu hii.

Naomba tukumbuke vile vile kubadilishana picha za tafrija tutakazofanya kwenye miji yetu katika kuadhimisha sikukuu hii ili iwe chahcu katika kuhamasishana.

Nawatakia nyote pasaka njema.

Mwenyekiti,
Jumuiya ya Watanzania Tamil Nadu.

No comments:

Post a Comment